Meya wa Jiji la Mwanza James Bwire aachiwa


Mwanza. Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire ameachiwa na Polisi waliokuwa wakimshikilia.

Akihutubia mkutano wa hadhara eneo la Nyakato leo Jumatatu Oktoba 30,2017 Rais John Magufuli amesema meya Bwire ameshaachiwa.

Ametoa kauli hiyo alipowaeleza wananchi kuwa  mabango waliyokuwa wameyabeba ameyaona likiwemo lililoeleza kuwa meya Bwire anashikiliwa na Polisi.

Awali, ilielezwa Bwire alishikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi kwa amri ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.

Hata hivyo, Mongella akizungumza na Mwananchi, alikana kutoa agizo kwamba meya huyo akamatwe.

Akizungumzia hilo, Mariam Lima ambaye ni katibu wa mitandao ya taasisi ya Alliance inayomilikiwa na meya Bwire alisema kuwekwa kwake ndani kulitokana na agizo la mkuu wa mkoa.

Comments