Mkutano Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (NEC), umefuta uchaguzi wa wenyeviti katika wilaya nne baada ya kubaini wagombea waliojitokeza hawakua na sifa.
Akitangaza uamuzi huo leo , Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, amezitaja wilaya hizo zilizofutiwa uchaguzi kwamba ni Moshi Mjini, Siha, Hai, pamoja na Makete.
Amesema sababu ya kufuta matokeo hayo ni kubainika kwamba wagombea waliojitokea hawakuwa na sifa, pamoja na kubainika kuwepo na viashiria hatarishi kwa chama.
Hivyo kutokana na uamuzi huo Polepole amesema kwamba wilaya hizo zitaanza upya mchakato wa uchaguzi huo.
Comments
Post a Comment