Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Mh. Joshua Nassari amefunguka na kusema ule ushahidi ambao walisema wanao kuhusu tuhuma za baadhi ya madiwani waliohama chama chao na kwenda CCM kuwa wamenunuliwa wataanza kuutoa siku ya kesho Oktoba 1, 2017.
Joshua Nassari amesema hayo kupitia ukurasa wake wa facebook na kusema kuwa anaamini kwamba Rais Magufuli atachukua hatua kwa kile kitakachoanza kuonekana kesho na kuzidi kusisitiza kuwa madiwani hao walinunuliwa na wali si kweli kwamba wamekwenda CCM na kukubali kazi inayofanywa na viongozi wa serikali ya awamu ya tano.
"Ni matumaini yangu kwamba Rais atachukua hatua kwa kile kitachoanza kuonekana kesho. Tulisema Madiwani hawaungi mkono juhudi za Rais, bali wanaunga mkono rushwa. Ushahidi hadharani kesho" alisema Joshua Nassari kupitia mtandao wake wa Facebook
Mbunge Joshua Nassari pamoja na Godbless Lema siku kadhaa zilizopita waliongea mbele ya waandishi wa habari kuwa wanaushahidi wa wazi kuwa baadhi ya madiwani ambao wametoka CHADEMA na kupokelewa CCM kuwa wamenunuliwa na kuhongwa rushwa na wateule wa Rais Mkoa wa Arusha.
Comments
Post a Comment