Siri Vijana wengi kukimbilia kusoma vyuo vya Nje ya Nchi


Wanafunzi zaidi ya 50 hapa nchini kutoka vyuo na shule mbalimbali wamepata fursa ya kwenda kusoma elimu ya juu nchini China kwa muda miaka 4.

Mkurugenzi wa kampuni ya Elimu solutioni Tanzania bwana Neithan Swed akiwa anawaaga vijana hao katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere leo  jijini Dar es salaam ameeleza kuwa vijana wengi hupitia kwenye kampuni hiyo kujiunga na vyuo vya nje kwa kuwa wanaamini mitaala yao inamjenga kijana kuwa na uwezo mkubwa mara baaada ya kuhitimu na kwamba mpango huo umeandaliwa mahususi kwa vijana wa kitanzania ambao wanandoto za kwenda kusoma ktika vyuo vikuu vya nje ya Nchi.

''Hivyo Kupitia mpango huu wa elimu solution wanafunzi watapata fursa kwani imezoeleka kupata elimu ya juu ni gharama kubwa  hivyo kupitia ufadhili wa gharama kidogo na mwanafunzi atakuwa chini ya uangalizi kuanzia siku anayo safiri mpaka China anakoenda kupata elimu yake.

Hii pia ni fursa kwa wazazi kujua kwamba kupitia mpango huu watoto wao watatimiza ndoto zao ikiwa amemaliza kidaoto cha nne au cha sita. Aliongeza

Mmoja wa wanafunzi hao Osmund Mbilinyi alisema kuwa yeye alikuwa na ndoto ya kwenda kusoma nje hivyo leo imetimia na kuwaasa wenye ndoto kama yake kutokata tamaa kwani kitu kinachowezekana pindi unapokua na nia.

Bi. Merrysponsa Nhwani mmoja wa wazazi wa watoto hao amesema kuwa amefurahishwa na fursa hiyo ambayo mtoto wake ameipata ya kwenda kusoma nje kwani ni moja ya mafanikio na ndoto ambayo alikuwa anaiota kwa siku zote.

Comments