Siwezi kuiomba radhi CCM - RPC Geita


RPC wa Geita,  Mponjoli Mwabulambo amefunguka na kusema yeye hawezi kuomba radhi kwa CCM mkoa wa Geita na kusema endapo itathibitika kweli amekidhalilisha chama hicho kama ambavyo wanadai baadhi ya viongozi mkoani humo yupo tayari kuacha kazi yake.
Mponjoli amesema kuwa yeye anaamini kila jambo alilofanya lilikuwa sahihi kwa kuwa viongozi hao walikuwa wanafanya uhalifu na kusema yeye anaona viongozi hao ndiyo walikuwa wakitaka kukudhalilisha Chama Cha Mapinduzi ila si yeye. 
"Siwezi kuomba radhi tena hilo nimethibitishie kabisaa niombe radhi kwa lipi mbona nimewaambia, mimi nidhalilishe Chama Cha Mapinduzi kwa lipi? Wao walisimama kama watetezi wa chama au watu wa kubomoa chama?" alihoji Mponjoli 
Mtazame hapa akifunguka zaidi  

Comments