"Wenye Ikulu ni nyinyi" - Magufuli


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Taifa, Dkt. John Magufuli amewapongeza wajumbe waliohudhuria Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM huku akiwataka watembee kifua mbele kwa kuwa Ikulu ni yao kwa maana bila ya wao yeye asingekuwepo hapo.
Baadhi ya wajumbe wa CCM
Dkt. Magufuli amesema hayo wakati akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano huo uliofanyikia katika kumbi za mikutano ndani ya Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Septemba 30, 2017 na kuendelea hadi Oktoba mosi mwaka huu.
"Kikao nimekifungua rasmi kuanzia muda huu, na niwathibitishie ndugu wajumbe kuwa Chama cha Mapinduzi ndiyo chama, hata vyama vingine vinayategemea matokeo mtakayofanya leo. Hiki chama ni imara kilicho asisiwa tangu za enzi ya Baba wa Taifa na tutaendelea kulisimamia taifa kwa manufaa ya taifa hili", amesema Dkt. Magufuli.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Taifa, Dkt. John Magufuli.
Pamoja na hayo Dkt. Magufuli ameendelea kwa kusema "Napenda kuwa karibisha kwa mara nyingine tena hapa Ikulu. Ikulu ni kwenu, wenye Ikulu ni nyinyi, tembeeni kifua mbele kwa sababu nyinyi ndiyo mliyonichagua mimi. Msingenichagua nisingeweza kufika Ikulu kwa hiyo mjione mpo katika nyumba yenu kama ilivyo nyumba ya watanzania wote", amesema Dkt. Magufuli.
Mtazame hapa chini Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Taifa, Dkt. John Magufuli akiendelea kuchanganua baadhi ya mambo.

Comments