kwa sasa kuna wimbi kubwa la watu ambao wanasumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume, wengi wao matatizo yao yanatumiika kwa kubadili mfumo wa maisha tu na wachache ambao wamejiharibu kwa kujichua na magonjwa mengine ndio wanaweza kuhitaji matibabu ya muda fualani.
katika tafiti zangu nimegundua yafuatayo ni chanzo cha kuishiwa nguvu za kiume, changamoto ambayo imeletwa na mfumo wa maisha.
1. Msongo mkubwa wa mawazo; nguvu za kiume na hamu ya kushiriki tendo hili huanzia kichwani mpaka kwenye uume wa binadamu, watu wenye misongo ya mawazo sababu ya kushindwa kutimiza wajibu wao wa kazi waliopewa kwa wakati, misongo ya mawazo sababu ya majukumu makubwa ya kifamilia ambayo yanakuja na huenda hakuna fedha za kukabiliana na hali hizo, msongo wa mawazo wa biashara zinazoyumba humfanya mwanaume asiweze kushiriki kabisa tendo la ndoa... omba msaada kama kazi zimekuzidi tafuta msaidizi kama umeajiajiri, kama waliokuajiri hawakuelewi tafuta kazi nyingine na uachane na hiyo kazi ya kufanya kazi usiku mpaka usiku lakini pia muda wa kazi ukiisha undoka kwenda nyumbani haraka kwenda nyumbani hakuna sifa ya kufanya kazi masaa mengi wakati mahusiano yako yanakufa.watu wanaofanya kazi benki ni wahanga sana wa matatizo haya.
lakini pia dawa zinazotolewa kutibu msongo wa mawazo huharibu nguvu hizi za kiume pia.
2. Ulevi wa kupindukia; unaweza kua unapenda kunywa pombe angalau kustarehe na kuonana na ndugu na jamaa lakini unywaji wa pombe kupitiliza ni hatari sana, humaliza nguvu za kiume na kukosesha hamu. habari njema ni kwamba pombe kidogo angalau pia moja mpaka mbili kwa siku ni nzuri kwa nguvu za kiume na afya ya moyo.
3. Dawa mbalimbali; baadhi ya dawa zinzotumika kwa shida mbalimbali au magonjwa mbalimbali zimethibitika kupunguza nguvu za kiume hasa zile zinazomezwa mara kwa mara au kila siku mfano dawa za presha, dawa za maumivu na dawa za msongo wa mawazo.
kumbuka usiache dawa kama una ugonjwa unaohitaji dawa kila siku sababu umesoma hapa, kwa upande mwingine uhai unaweza kua muhimu kuliko nguvu za kiume.
4. kufikiria sana; huwezi kupata nguvu za kiume kama unafikiria mambo mengi yanayokuathiri labda maumivu ya vifo ya wapendwa, maumivu ya kuachishwa kazi, maumivu ya kusalitiwa na mpenzi au kuachwa, na uchovu sana wa shughuli za kila siku. jaribu kurelax, kukubali matokeo, kupata usingizi wa kutosha na kushiriki mazoezi na kumbuka mazoezi yakiwa makali sana humaliza nguvu za kiume.
5. Hasira; hasira juu ya mwenzi wako au mtu yeyote aliyekukwaza hufanya ushindwe kushiriki tendo la ndoa, hakikisha unamwambia mpenzi wako mambo yanayokukwaza...kuyaweka moyoni haitakusaidia hata kidogo.
6. Wasiwasi; wanaume wakishapata matukio kadhaa ya kuadhirika na kushindwa kufanya tendo la ndoa huanza kuogopa kukutana tena na mwanamke kwa hofu kwamba wataadhirika tena...tafuta chanzo ni nini na urekibishe, huenda siku hiyo haukua vizuri au ulikua na njaa...kisha jiamini kwamba sasa ntafanikisha.
7. Vitambi na unene; vijana wengi kwanzia miaka 30 mpaka 40 hilo ndio tatizo lao kubwa, yaani kukosa nidhamu ya kupambana na ungezeko la miili yao na matokeo yake uume hua mdogo na nguvu kidogo sana lakini pia ulaji wa vyakula vya haraka kama chips na mikaango mbalimbali wakati wa kazi na kusahau vyakula asilia kama mihogo,karanga, ugali,wali, matunda na mboga za majani...asikudanganye mtu kama umeshindwa kupungua uzito nguvu za kiume utazisikia redioni.
8. kutojiamini; baadhi ya wanaume hushindwa kujiamini kwa kujikosoa vitu mbalimbali vilivyoko kwenye miili yao ambavyo wakati mwingine hata mwanamke mwenyewe havijali sana mfano kuhisi ana uume mdogo sana wakati uume wake ni wa kawaida, kuhisi hana mwili mzuri na kadhalika.
9. Kukosa hamu ya tendo la ndoa; kwa maisha ya sasa hii husababishwa na kuchoka sana na kazi na kukosa muda wa kupumzika, kuna watu wanafanya kazi kila siku ya maisha yao kwa madai wana roho za kichaga...hizo pesa unazotafuta huku unaharibu afya hazitakusaidia kwa lolote hata ukizipata mwisho wa safari na utaibiwa mke na walafi wa mtaani.
10. Magonjwa; haya ni magonjwa mbalimbali ambayo hua hayaponi au huchukua muda sana kupona kwa namna moja au nyingine huharibu nguvu za kiume moja kwa moja mfano kisukari, presha, ajali za migongo na magonjwa ya mishipa ya fahamu, madonda ya tumbo, kifua kikuu, pumu na kadhalika...
Mwisho; unaweza kua unaona aibu kuongea na daktari kuhusu tatizo lako lakini kimya chako hakitakusaidia, jaribu mwenyewe kufikiri chanzo ni nini ili uweze kubadili mfumo wako wa maisha kama kupunguza uzito, kupunguza kazi na kuishi kwa uwezo wako wa kifedha,kuacha kutumia dawa zinazoharibu nguvu zako, kupunguza ulevi na hata kupata matibabu kama ikionekana ni muhimu
Comments
Post a Comment