Maimartha amfungukia Mobeto



MTANGAZAJI maarufu Bongo, Maimartha Jesse ameibuka na kusema ataendelea kumfunda mwanamitindo Hamisa Mobeto ingawa amemjibu vibaya, kwani alichoamua ni kumshauri kwani anaona anakoelekea siko.

Akiongea na Risasi Jumamosi, Maimartha alisema kuwa alimshauri Hamisa kuwa makini kwani kuwa mgeni rasmi kwenye tamasha la Gal Power lililofanyika Uganda hivi karibuni halikuwa na hadhi yake na ilionekana yupo kwenye kushindana na Zarinah Hassan ambaye hamuwezi.


“Kiukweli niliamua kumshauri na nitaendelea kumshauri ingawa alinijibu vibaya, lakini naamini ujumbe umemfikia na anatakiwa ajirekebishe na lile tamasha halikuwa na hadhi yake,” alisema Maimartha.

Hata hivyo, Maimartha alisema ataendelea kuwapa Kitchen Party mastaa mbalimbali ambao wanaonekana kwenda kinyume na wanavyotakiwa kuwa na anaomba watu mbalimbali wanaokerwa na tabia zao wapige kelele za kupinga ili zisiendelee.

Comments