- Get link
- X
- Other Apps
BIFU zito linatokota katika kikosi cha Arsenal kati ya Alexis Sanchez na baadhi ya wachezaji wenzake, ambao wanataka aondoke klabuni hapo.
Ugomvi kati ya Sanchez na wenzake ulianza kwenye mechi dhidi ya Southampton, mwanzoni mwa mwezi huu.
Katika mchezo huo, ambao Arsenal ilitoka sare ya 1-1 inasemekana nyota wenzake hawakufurahishwa na kiwango cha Sanchez na hasa alivyokuwa anapoteza mipira mara kwa mara.
Nyota aliyejitolea kumpa makavu Sanchez alikuwa Jack Wilshere, ambaye alimlaumu kwa kucheza ovyo.
Sanchez inadaiwa amekuwa na uhusiano mbovu na nyota wenzake, ambao wanatamani aondoke Januari hii.
Kali ya yote ilikuwa Alhamisi iliyopita wakati baadhi ya mastaa wa Arsenal walipogoma kwenda kushangilia na Sanchez alipofunga kwenye mechi dhidi ya Crystal Palace, ambayo Arsenal ilishinda mabao 3-2.
Wenger alikwepa kuzungumzia suala hilo alipoulizwa na waandishi wa habari.
“Sikuona kwa kweli kilichotokea baina ya wachezaji wangu,” alisema Wenger, ambaye timu yake inakabiliana na West Bromwich leo.
Mtu mmoja ndani ya klabu hiyo alidai kuwa Sanchez ni mkorofi na ni ngumu kuishi naye.
Wenger inasemekana ameingiwa na wasiwasi kuwa chuki dhidi ya Sanchez inaweza kuyumbisha timu hiyo.
Kuna taarifa kuwa anaweza kumuuza kwenye dirisha dogo ingawa Sanchez anataka amalize msimu ili aondoke bure na kujiunga na Manchester City
Comments
Post a Comment