Tapeli avunja rekodi ya kuhukumiwa miaka mingi Jela Thailand




Mahakama moja ya Thailand imemuhukumu tapeli mmoja zaidi ya kifungo cha miaka 13,000 jela.

Pudit Kittithradilok ,34, alikiri kumiliki mradi mmoja wa piramidi ambao aliwaahiidi wawekezaji kupata mapato ya hali ya juu.

Takriban watu 40,000 walikubali kuwekeza kiwango cha $160m katika kampuni yake.

Mahakama ilisema kuwa alijihusisha na vitendo vya kutoa mikopo na makosa 2,653 ya udanganyifu.

Baada ya kukiri ,mahakam hiyo ilipunguza hukumu hiyo na kumpatia kifungo cha miaka 6,637 na miezi sita.

Huenda asihudumu zaidi ya miaka 20 kwa kuwa sheria ya Thai inatoa miaka 10 kwa makosa mawili aliyopatikana nayo.

Waendesha mashtaka waliambia mahakama kwamba Pudit aliandaa semina ambapo waliohudhuria walishawishiwa kuwekeza katika kile alichosema ni biashara zinazohusiana na ujenzi ,urembo, uuzaji wa magari yaliotumika uuzaji wa bidhaa nje ya nchi miongoni mwa vitu nyengine.

Kulingana na gazeti la Bangkok Post, wawekezaji waliahidiwa mapato makubwa na marupurupu iwapo wataleta wanachama wapya.

Na kama mradi mwengine wowote wa Piramidi, wawekezaji waliowekeza fedha zao wa kwanza wanalipwa kuwalipa wanachama wao wa kwanza.

Pudit alikuwa anazuiliwa katika jela ya Bangkok tangu alipokamatwa mwezi Agosti wakati aliponyimwa dhamana.

Mahakama ilizipiga faini kampuni zake mbili ilio sawa na dola milioni 20 kila moja.

Pudit na kampuni zake aliagizwa kulipa takriban dola milioni 17 kwa waathiriwa 2,653 pamoja na riba ya kila mwaka ya 7.5%

Comments