- Get link
- X
- Other Apps
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Michael Isamuhyo amesisitiza upendo na mshikamano katika Jeshi hilo.
Akizungumza katika hafla maalumu ya kumuaga iliyofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari Jitegemee amesema siri ya mafanikio yake Jeshini imejengwa na nguzo ya upendo na mshikamano.
Amesema kufikia Januari 31 saa 6:00 usiku atakuwa anastaafu rasmi nafasi hiyo hivyo kutoa nafasi kwa kiongozi mwingine kuiongoza.
“Ninachowaambia wana JKT ni kumpa ushirikiano kiongozi ajaye ili kuendeleza misingi thabiti iliyojengwa na Jeshi hili tangu kuanzishwa kwake.
“Kukosa kunipa ushirikiano na kusikilizana nisingefika hapa leo, niwaombe sana, mshikamane naye na mfanye naye kazi kwa upendo ”amesema Meja Jenerali Isamuhyo.
Ametaja kitu ambacho atakikumbuka akiwa nje ya Jeshi hilo kuwa ni upendo na mshikamano aliokuwa akipewa muda wote alipokuwa kiongozi.
“Unajua Jeshini huwa tunakuja mmojammoja tukifika tu, tunajumuishwa kwenye makundi na kuanzia hapo hufanya kazi kwa ushirikiano.
“Nilikuja nikiwa kijana kabisa, nitakuwa mpweke sana nikiwakumbuka wenzangu ambao nilifanya nao kazi pamoja, ambao wakati huo watakuwa kwenye majukumu mengine Jeshini na mimi nikiwa uraiani, ”amesema Meja Jenerali Isamuhyo
Isamuhyo amefafanua kuhusu utendaji katika Jeshi hilo lenye jukumu la kujenga vijana na uchumi kuwa upo imara.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mipango na Maendeleo wa JKT Kanali Festus Mang’wela amemzungumzia Isamuhyo kama kiongozi aliyeitumikia kwa weledi na mafanikio nafasi yake.
Amesema kwa kipindi alichokuwa nao ameweza kuongeza vikosi vitano vya vijana wa kujitolea wa JKT.
“Ameongeza nafasi kwa vijana wa kujitolea wa JKT kwa vikosi vitano ambavyo ni Itaka kilichopo mkoani Songwe, Makuyuni kilichopo mkoani Arusha, Luwa na Mirundikwa vilivyopo mkoani Rukwa na Mpwapwa kilichopo mkoani Dodoma.
“Hili kwetu kama taifa ni la kujivunia kwa sababu amewapa vijana nafasi ya kujitolea katika Jeshi la Kujenga Taifa, lakini pia ameacha miradi mbalimbali ikiwamo imekamilika na mingine inaendelea kukamilishwa, ”amesema Kanali Mang’wela.
Naye Kanali Hawa Kodi Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, alimzungumzia kiongozi huyo kuwa alikuwa ni mzazi na mwalimu.
Amesema “Tulipokosea alituelekeza kwa upendo, alikuwa mtu wa watu akihakikisha mahitaji muhimu yanapatikana na kila suala linapatiwa ufumbuzi, ”amesema Kanali Kodi.

Comments
Post a Comment