Dunia imekuwa ikihaha kila siku kutafuta suluhu na kukomesha biashara haramu ya dawa za kulevya, ambazo zimekuwa zikiangamiza vijana kwa asilimia kubwa sana duniani kote.
Madawa haya ambayo yapo mbali mbali duniani lakini yakiongozwa na cocaine kwa umaarufu, yamekuwa na madhara makubwa huku watu maarufu duniani wakipoteza maisha kwa matumizi yake, wengine kubaki na ulemavu huku watu mbali mbali wakijiingizia kipato kikubwa kwa kufanya biashara ya kuyauza.
Leo nakuletea historia ya madawa ya kulevya aina ya cocaine ambayo hata nchini kwetu huwa yanapatikana ingawa ni kosa kisheria kukutwa nayo.
Madawa ya Cocaine yametokana na mmea unaojulikana kama 'coca' ambao unapatikana kwa wingi katika nchi za Kusini mwa Amerika. Mmea huu ulikuwa ukitumika kama kiburudisho kwa watu wa jamii hizo wanapotafuna, kwa kusisimua miili yao na kufanya kuchangamka, hususani wakati wa sherehe mbali mbali, kutokana na nutrients ambazo unao.
Baada ya Waspain kuingia Marekani ya Kusini walikuwa wakipuuzia habari za jani hili la coca na kusema ni jambo la kishetani. Lakini baada ya kugundua ni ukweli walianza kuliruhusu kulitumia na hata kulipia kodi, na kuanza kupiga hatua kwa kuweka kwenye sigara wakati wa kuvuta.
Ingawa kazi ya mmea wa coca kujulikana kwa muda mrefu, hawakuweza kutenganisha nutrients yake kutokana na kukosekana kwa teknolojia, mpaka mwaka 1833. Baadhi ya Wanasayansi wa Uingereza walijaribu kufanya hivyo lakini walishindwa kutokana na kutokuwa na utaalamu zaidi wa masuala ya kemia.
Kwa mara ya kwanza kileo cha cocaine kiliwezekana kutenganishwa kwenye jani la coca na Mkemia wa Ujerumani, Friedrich Gaedcke mwaka 1855, na kuipa jina la 'erythroxyline' lakini haikuwa na impact kubwa sana.
Mnamo mwaka 1856 Mkemia Friedrich Wöhler alimuomba Dkt. Carl Scherzer kumletea majani ya coca kwa wingi kutoka Amerika yya Kusini alikokwenda. Mwaka 1859 meli ya aliyokuwa akisafiria Scherzer ilitia nanga na mzigo wa majani ya coca, na kisha Mkemia Wohler kumpatia mwanafunzi aliyekuwa akisomea PHD ya masuala ya Kemia, Albert Nieman, kulifanyia kazi jani hilo.
Nieman alielezea hatua zote alizozipitia katika kutenganisha jani hilo na nutrients yake ambayo ndiyo 'cocaine', kwenye kitabu cha (On a New Organic Base in the Coca Leaves) ambacho kilikuwa published mwaka 1860, na kumpatia PHD yake.
Baada ya hapo watu mbali mbali waliendelea kufanya tafiti zao juu ya cocaine na kugundua mambo mbali mbali ikiwemo madhara yake.
Mwaka 1885 kampuni kubwa ya madawa ya Parke-Davis ilianza kuuza cocaine kwa njia mbali mbali ikiwemo wenye sigara, unga na hata mcanganyiko ambao unaweza ukawa injected moja kwa moja kwa njia ya sindano kwenye mwili wa binadamu, ambapo mpaka sasa madawa hayo yanaendelea kutumika kwa kasi kubwa sana.
Majani ya coca
Albert Nieman aliyetenganisha cocaine kwenye jani la coca ambayo bado inatumika mpaka sasa.
Friedrich Gaedcke mwanasayansi wa kwanza kutenganisha cocaine kutoka kwenye jani la coca.
Wananchi wa Marekani ya kusini wakitafuna jani la coca
Comments
Post a Comment