- Get link
- X
- Other Apps
MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya, Inspekta Haroun ameeleza kwamba wanaosema wanamuziki wakongwe wameshindwa kimuziki na wasanii wanaochipukia ni uongo kwani wao bado wako vizuri tatizo ni mfumo wa maisha tu umebadilika.
Akipiga stori na Risasi Vibes, Inspekta Haroun alisema wasanii wengi wa zamani wako kimya kwa ajili ya kujipanga zaidi kwa sababu muziki wa sasa siyo sawa na ule wa zamani kila kitu kimebadilika na wanamuziki wanaongezeka kila kukicha.
“Unajua muziki umebadilika sana siyo sawa na vile tulivyokuwa tunafanya zamani kwanza gharama tu za studio kwa sasa ni kubwa lazima mtu ujipange pia kwenye nyimbo lazima tuwaze sana tunaimba nini maana wasanii wengi wa muziki siku hizi wanatoa nyimbo zinakufa kwa kuwa hawajipangi sawasawa.
“Nilikuwa kimya kwa sababu nilikuwa najipanga vizuri na sasa narudi rasmi kwenye gemu na hakuna mwanamuziki yeyote wa sasa anayeweza kutushinda sisi wakongwe maana muziki wao ni mwepesi sana na haudumu kwa muda mrefu lakini nyimbo zetu tulizoimba enzi zile zikipigwa sasa bado zinawika na zina ujumbe wa maana,” alisema Inspekta Haroun.
Comments
Post a Comment