NA MWANDISHI WETU
Kamati mbalimbali za maendelea kupitia
kikao cha baraza la madiwani katika halimashauri ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga
pamoja na wataalam zimewakilisha taarifa za utekelezaji wa miradi ya robo mwaka
katika kipindi cha mwaka 2018.
Kupitia uwasilishaji huo wa taarifa
sekita ya elimu imebainika kuwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na
upungufu wa madarasa ,meza na viti huku kukiwa na mjadala wa wanafunzi watano
waliopatiwa mimba wanaosoma shule ya sekondari ya baba khaji iliyoko kata ya
busoka wilayani kahama mkoani shinyanga jambo ambalo limempelekea afsa elimu
sekondari kushindwa kutolea ufafanuzi juu ya hatua stahiki zilizochukuliwa kwa
wahusika waliosababisha na waliopewa mimba
Kwaupande wake diwani wa nyihogo Mh Shadraki
na diwani wa Kahama mjini Mh Hamidu Kapami wamehoji juu ya swala la kuzagaa kwa
mifugo mjini kutokana na mifugo hiyo kuwa kero kwa wananchi na
wafanyabiashara ambapo Mkurugenzi
mtendaji wa halmashari hiyo bwana Anderson Musumba amesema tayari wameanza kuchukua hatua ili kuhakikisha
wanaondoa mifugo yote inayo zunguka na kuwataka wafugaji kuwa na vibali vya
kufuga huku akipiga marufuku ufugaji wa nguruwe mjini.
Katika hatua nyingine baraza limemtaka
mkurugenzi kuhakikisha analitafutia ufumbuzi eneo la mlima lililopo shunu juu ya uhalali wake ili kuondoa mgogoro kati
ya wananchi na serikali.
Comments
Post a Comment