Meek Mill aachiwa kwa dhamana, atinga kwenye game ya Sixers VS Miami




MAHAKAMA Kuu ya Pennysylvania juzi iliamua kuachiwa kwa dhamana kwa mwanamuziki (rapa) Meek Mill. Mwanamuziki huyo ambaye jina lake halisi ni Robert Rihmeek Williams (30), mnamo Novemba mwaka jana, alihukumiwa kifungo cha miaka miwili hadi minne jela kwa kuvunja masharti ya kutofanya makosa na kukiuka kanuni akiwa chini ya uangalizi ‘probation’ kama ilivyokubaliwa baada ya kukamatwa akiwa na madawa ya kulevya na bunduki mwaka 2008.

Kesi hiyo ya Mill imeibua shutuma kubwa dhidi ya mfumo wa haki kwa wahalifu na inavyotumiwa kwa Wamarekani wenye asili ya Afrika. Kufungwa kwake kulisababisha wimbi la malalamiko kutoka kwa watu maarufu kama Kevin Hart, Colin Kaepernick na Jay-Z ambaye aliandika katika gazeti la New York Times kwamba tukio hilo ni “mfano mmoja tu wa mfumo wa haki kwa wahalifu ambao hutumiwa kuwanyanyasa mamia kwa maelfu ya watu weusi kila siku”.

Mahakama hiyo ya juu zaidi ilifutilia mbali uamuzi wa Jaji Genece Brinkely ambaye alimkatalia dhamana Mill wiki iliyopita baada ya ofisi ya mwanasheria wa wilaya ya Philadelphia kutaka hukumu ya mwanzo kuhusiana na madawa ya kulevya ifutwe.

Wafuasi wa Mill walifurika katika mahakama hiyo wakitaka aachiwe. Miongoni mwao alikuwamo mtoto wa kiume wa Mill na mama yake, ambapo walisema kwamba, kwa mujibu wa jarida la Phiadelphia, ofisa aliyemkamata Mill alikuwa katika orodha ya polisi “wenye majina machafu na wasiostahili kufanya kazi katika ofisi ya mwanasheria wa wilaya”.

Baada ya kuachiwa, Rapa Meek Mill aliwasili Wells Fargo Center kuangalia timu yake ya Sixers ikicheza Game 5 dhidi ya Miami Heat ambapo matokeo yalikuwa Sixers 104 – 91 Miami Heat.

Joel Embiid– Pts 19,Reb 12
Ben Simmons — Pts 14, Reb 10
J. J. Redick — Pts 27
Aggr : 4 – 1
Sixers wamefuzu Round 2.

Comments