Pretty Kind afunguka kifo cha Masogange champa funzo




MSANII wa muziki na filamu Bongo, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ ameibuka na kueleza kwamba kifo cha mrembo, Agness Gerald ‘Masogange’ kilichotokea wiki iliyopita kimempa funzo kubwa katika maisha yake na kimemsababisha azidi kubadili tabia na mwenendo wake zaidi.

Akizungumza na Za Motomoto News, Pretty Kind alisema kifo hicho kimempa funzo kwani hapishani sana umri na Masogange hivyo kimemwaminisha kwamba kufa kunakuja wakati wowote haijalishi una umri mkubwa au mdogo kwa hiyo amejikuta akizidi kubadilika na kuachana na maisha ya starehe yasiyompendeza Mungu.

“Kifo cha Masogange kimeniumiza sana mpaka niliugua ghafla na kushindwa hata kwenda kuuaga mwili wake pia kimenipa funzo kubwa maana maisha aliyokuwa anaishi ndiyo nilikuwa naishi mimi zamani kabla sijaanza kubadilika, nilikuwa naishi maisha yasiyompendeza Mungu, kujiachia kwa sana lakini kwa sasa nimezidi kubadilika kutokana na kifo hiki muda mwingi natumia kumuomba Mungu na kufanya kazi kwa bidii maana kifo kipo wakati wowote,” alisema Pretty Kind.

Comments