Watu 18 wauawa kikatili wakiwa Kanisani




Kutoka nchini Nigeria, watu 18 wameuawa kikatili jana April 24, 2018 wakiwa kanisani jambo ambalo Rais Muhammadu Buhari amelilaani na kusema ni la ‘kishetani‘.

Kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi Benue katika mji wa Makurdi, Fatai Owoseni, takribani wanaume 30 ambao ni wachunga mifugo walivamia na kuwaua watu hao 18, wawili kati yao wakiwa viongozi wa kanisa.

 Wauaji hao wanaripotiwa kuvamia eneo hilo la kanisa ambapo kulikuwa na misa ya mazishi ilikuwa ikiendelea na kuanza kuwashambulia watu pamoja na wachungaji hao ambao walikuwa wanaongoza misa hiyo.

Comments