Viongozi wa CCM Tarime wahojiwa na Polisi kwa masaa 3



Viongozi wa kamati ya siasa  CCM ngazi ya Wilaya wamewataka wananchi waishio katika vijiji vinavyopakana na hifadhi ya taifa ya Serengeti waliotakiwa kutoka katika eneo hilo kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki ambacho bado wanaendelea kuhakikisha wananchi hao wanapata haki ikiwemo kutohamishwa bila kujua wapi pakwenda.

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime Mh Daudi Ngicho wakati akiongea na waandishi wa habari ogisini kwake nakusema kuwa yeye kama kiongozi wa ccm Wilaya atahakikisha anasimamia na kuwatetea wananchi wanyonge wanaoteseka kutokana na utaratibu wa baadhi ya watumishi kutowasikiliza wananchi wanaowaongoza katika kutatua migogoro ya Ardhi.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kupokea taarifa kutoka kwa baadhi ya wananchi mbali mbali juu ya zoezi la uwekaji wa alama katika vijiji vinavyopakana na hifadhi kutakiwa kukaa eneo la hifadhi jambo ambalo halikuwashirikisha  wananchi husika jambo ambalo limepelekea viongozi hao kufika na kukagua eneo hilo nakuamuru wasitoke eneo hilo mpaka wapate ufafanuzi wa kina  nakuhaidi kushirikiana nao  bega kwa bega  katika kuhakikisha haki inapatikana

Nao wakazi wa maeneo hayo wameeendelea kuwashukuru viongozi wa ccm ngazi ya Wilaya kwa kuonyesha moyo wa dhati katika kuwahudumia wananchi huku kuwaomba kutobadilika na kuendelea kuwa shupavu kama rais wa Mh john pombe magufuli

Aidha Mkaruka Kura ambaye ni katibu  wa ccm wilayani hapa ameongeza kuwa kwa kufanya hivyo wameweza kuitwa na jeshi la polisi ili kutoa ufafanuzi huku wakidhaniwa kuwa viongozi hao walienda kufanya mkutano wa hadhara na wananchi wa eneo hilo jambo ambalo ni kukiuka utaratibu ambapo wamedai kuwa waliamua kuongea na wananchi baada ya kuwakuta wamekusanyika huku wananchi hao wakizuia njia nakuwataka wasikilize Kero zao.

Comments