Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amedai kitendo mchezaji, Cristiano Ronaldo kununua gari aina ya bugatti lenye thamani ya bilioni nne za kitanzania ni ukatili uliopitiliza bora pesa hizo zingetumika kulipa wachezaji wa Yanga, Simba na Azam
"Bugatti ya 2017 imenunuliwa na Ronaldo kwa thamani ya Dola milion 1.8, karibia na Bilioni nne za madafu. Unalipa 'salary' ya mwaka mzima kwa wachezaji wa Yanga, Simba na Azam. Huu ni ukatili uliopitiliza", ameandika Manara.
Comments
Post a Comment