Kigwangalla kuja na utalii wa 'Entertainment'


Waziri wa Maliasili na Utalii Dr. Hamisi Kigwangalla ameagiza taasisi zote zilizopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuwekeza kwenye mkakati wa kuleta utofauti katika vivutio vya utalii.

Waziri Kigwangalla ametoa agizo hilo jijini Arusha, kwenye kikao chake na wafanyakazi wa TANAPA ambapo amesema, lengo la wizara yake ni kuongeza idadi ya siku na kiasi cha fedha ambazo mtalii atatumia akiwa nchini.

Pamoja na watalii kutoka nje, lakini waziri ameagiza mamlaka zinahakikisha vivutio vya utalii lazima viwahusishe wananchi wa maeneo husika ili kuongeza idadi ya watalii wa ndani.

Aidha katika kikao hicho waziri ameeleza kuwa, wizara yake inataka kuwekeza kwenye utalii wa "Entertainment" ambao utahusisha fukwe mbalimbali katika miji iliyopo katika ukanda wa bahari na maziwa.  "Utalii wa Entertainment yaani burudani, tuna fukwe mbalimbali ambazo zinaweza kuleta impact kubwa kwenye sekta hii na kutengeneza ajira kwa vijana" amesema Waziri Kigwangalla.

Ameongeza kuwa utalii wa burudani utaambatana na utalii wa utamaduni ambapo wizara iko mbioni kuanzisha Dar Bus Tour, Arusha Bus Tour, Presidential Museum, Theme Park, Tanzania na Heritage Month.

Comments