NA MWANDISHI WETU
Kutokana na kuwepo kwa
changamoto nyingi katika sekta ya elimu wilayani Kahama mkoani Shinyanga mkuu
wa wilaya ya Kahama bwana fadhili nkulu amekutana na mwakilishi mkazi wa umoja
wa mataifa hapa nchini bw Alvaro Loadregers na kufanya mazungumzo juu ya kupata
msaada wa utatuzi wa changamoto hizo ikiwa ni pamoja na mimba,upungufu wa
madarasa, upungufu wa meza na madawati , vitabu na mahitaji mengine muhimu katika
shule mbalimbali Wilayani humo.
Hayo ameyasema leo
ofisini kwake alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari kuwa bwana Loadregers amekubaliana na maombi
hayo na kumwahidi February mwaka huu
yeye pamoja na timu yake watakuja Kahama ili kujionea changamoto zilizoko
shuleni nakuanza kuzipatia ufumbuzi.
Pia Nkulu amewahimiza
wazazi ambao bado hawajawapeleka watoto wao shuleni kipindi hiki cha masomo
kufanya hima kuwapeleka wakapate haki yao ya msingi kabla serikali haijachukua
sheria juu yao.
Akizungumzia swala la
maendeleo kwa upande wa afya amesema wamejipanga kuendelea kuboresha katika ujenzi wa zahanati na vituo vya afya
katika halmashauri zote huku akiwapongeza wakurugenzi wa halmashauri zote
kwajitihada nzuri katika kupigania maendeleo ya wananchi na wilaya.
Comments
Post a Comment