Alphonse Areola:Nina wasiwasi juu ya Neymar niliona alivyoumia




Baada ya nyota wa PSG Neymar Jr kuumia kwenye mchezo wa jana usiku ligi kuu ya Ufaransa kati ya timu yake dhidi ya Marseille, mlinda mlango wa PSG Alphonse Areola amesema anawasiwasi na kuumia kwake.

Katika mchezo huo ambao PSG ilishinda kwa mabao 3-0, Neymar alitolewa kwa Machela baada ya kuumia kifundo cha mguu huku akiacha hofu kama atakuwa tayari kurejea dimbani kabla ya mchezo wa UEFA dhidi ya Real Madrid Machi 6.

"Nina wasiwasi juu ya Neymar, niliona alivyoumia mguu wake na ulivimba hapohapo," amesema Areola. Golikipa huyo ameongeza kuwa Neymar ni mchezaji muhimu kwenye timu hivyo wanamatumaini atarudi karibuni.


Kwa upande wake kocha wa PSG Unai Emery amesema Neymar atapona kabla ya mchezo wao wa marudiano dhidi Real Madrid ambao utapigwa kwenye uwanja wa Parc des Princes.

PSG inaongoza ligi ikiwa na alama 71, tofuati ya pointi 14 na timu inayoshika nafasi ya pili Monaco yenye alama 57, huku Marseille ikiwa katika nafasi ya tatu na alama 55.

Comments