Heri Muziki afunguka hataki tena kuwa katika Mahusiano na mtu maarufu




Muimbaji wa Bongo Flava, Heri Muziki amesema baada ya kuachana na aliyekwa mpenzi wake, Diva hatarajii tena kuwa katika mahusiano na mtu maarufu.

Hitmaker huyo wa ngoma ‘Cheche’ ameimbia Bongo5 kuwa baada ya kuachana na Diva ndio itakuwa mwisho wa yeye kuingia katika mahusiano na mtu maarufu.

“Sikuwa nime-date na mtu maarufu before, wakwanza ni yeye, kwa hiyo baada yaku-date naye imekuwa ni experience kwangu, after that nisingependa ku-date na mtu maarufu tena,” amesema.

Baada ya kuachana kwao kulipelekea Diva kutoa sauti ya Heri Muziki katika wimbo ‘Waambie’ ambao Heri alifanya kwa kushirikiana na Mr. Paul pamoja na Mwana FA na Diva kuweka sauti pale alipoondoa sauti ya Heri Muziki.

Comments