Maktaba yaja na mbinu mpya ya Wanafunzi kujua kusoma




Maktaba ya Mkoa wa Mtwara imeanzisha programu mpya ya kuwasaidia wanafunzi wasiojua kusoma, kuhesabu na kuandika (KKK) kuhakikisha wanakuwa na uelewa mpana.

Mkutubi Msaidizi wa Maktaba ya Mkoa wa Mtwara, Fred Mpoma alisema juzi wakati wa uzinduzi wa kusoma kwa kutumia maktaba mtandao.

Mpoma alisema kuwa shule nyingi zina uhaba wa vitabu vya kuwafundishia wanafunzi na hivyo ujio wa maktaba mtandao katika maktaba hiyo utasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto ya upungufu wa vitabu katika shule za msingi mkoani hapa.

“Tumeona shule nyingi za hapa hazina uwezo wa kununua vitabu kutokana na bajeti zao kuwa ni ndogo lakini kio –kiti (maktaba mtandao) itawasaidia walimu kupata vitabu ambavyo wanavihitajika kufundishia,” alisema.

Mwalimu wa Shule ya Msingi Rahaleo, Hilda Mapunda alisema maktaba mtandao itakuwa msaada mkubwa kwao kwa ajili ya kuongeza ustadi wa kusoma kwa watoto hususan wa madarasa ya chini.

Comments