WAZIRI AAGIZA AFSA ARIDHI KAHAMA AKAMATWE AFIKISHWE MAHAKAMANI.

Waziri wa aridhi nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi  ameagiza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kwakushirikiana na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kuhakikisha inawakamata na kuwafikisha mahakamani watendaji wa idara yaardhi kwa kusababisha migogoro ya ardhi wilayani humo akiwemo aliyekuwa afisa aridhi mteule  bw Charles kitalya na kwamba  asakwe na kukamatwa mahali popote alipo afikishwe mahakamani.

Agizo hilo limetolewa  leo baada ya waziri huyo kupokea  taarifa ya maeneo mengi ya migogoro wilayani humo kusababishwa nab w kitalya ikiwemo eneo la serikali linalo milikiwa na chuo cha maendeleo ya jamii mwanva,eneo la baferson igomelo,na kuuza eneo la soko la vumilia.

Katika hatua nyingine ameiagiza idara ya ardhi kushirikiana na makampuni binafsi ya upimaji kuhakikisha wanawapimia wananchi maeneo yao ili kuupanga vizuri mji wa kahama na wakazi waweze kulipa kodi za aridhi na majengo.

Pia lukuvi amewataka wafanyakazi wa halmashauri zote nchini kujitasimini katika utendaji wao hukuakiongeza kuwa serilikali ya awamu ya tano inahitaji kila awae kutenda kazi kwauadilifu mkubwa na uaminifu.

NA NYAMITI ALPHONCE NYAMITI

Comments