Wema Sepetu afanikiwa kupata akaunti yake ya Istagram



Muigizaji wa filamu mwenye nyota yake bongo na Afrika Mashariki Wema Sepetu, amefunguka na kusema amejisikia vizuri na furaha kwa yeye kurudi kwa mara nyingine katika mitandao ya kijamii.

Wema amebainisha hayo asubuhi ya leo baada ya kukabidhiwa ukurasa wake wa kijamii instagram na watu waliokuwa wanamhangaikia kuupata tokea waharifu kuuiba kwa takribani mwezi mmoja sasa.

"Alhamdulillah nimerudi tena, huu wakati ni kweli. Namshukuru sana Tizzo, daah nime-miss kweli ukurasa wangu. Najua jinsi mlivyoni-miss kwa sana. 'But it feels good to be back", amesema Wema. 

Kutokana na hilo, wapenzi na mashabiki wa Wema Sepetu wamepokea ujumbe huo kwa shauku kubwa huku wengine wakimpa maneno yenye faraja kutoka na kupotea mitandaoni kwa kipindi kirefu kidogo.

Comments