78 wapoteza maisha katika moto


Watu 78 wameripotiwa kupoteza maisha baada ya moto kuwaka katika kituo cha polisi nchini Venezuela.

Kwa mujibu wa habari wanamume 68 na wanawake 10 ndio waliopoteza maisha.

Moto huo umezuka baada ya wafungwa kuwasha vitanda vyao moto kama njia ya kutaka kutoroka.

Tukio hilo limetokea katika mji wa Valencia in Carabobo .

Uchunguzi zaidi unafanyika.

Comments