CRDB YAUNGA SEKTA YA AFYA


NA MWANDISHI WETU
Bank Ya C.R.D.B  Tawi La Kahama Kwa kutambua Jitiahada Za Serikali  Ya Awamu Ya Tano Wameamua Kuunga Mkono Katika Sekita Ya Afya Kwakutoa Tsh Milioni 8 Zitakazotumika Katika Ukamilishaji Wa Jingo La Zahanati Na Nyumba Ya Mganga Kwenye Zahanati Ya Kijiji Cha Kangeme Kata Ya Ulowa Katika Halmashauri Ya Ushetu.

Akikabizi Hundi Ya Pesa  Hizo Meneja Wa Tawi Hilo Bw Luther Mneney Amesema Kutokana Na Jitihada Za Rais Magufuli Wamechukua Uamuzi Huo Kuungana Na Serikali Kusaidia Sekita Hiyo Muhimu Kwa Nchi Ya Viwanda.


Pia ameitaka Jamii Kuanza Kutunza Pesa Kwa Mfumo Wa Kibenki Utakao Wawezesha Kujikwamua Pindi Changamoto Zinapojitokeza Nakuongeza Kuwa Ili Kupata  Maendeleo Lazima Wajue  Kutunza Kabla Ya Kutumia.

Nae Naibu Waziri Wa Ujenzi Mh John Kwandikwa Ameupongeza Uongozi Wa Banki Hiyo Kwakutambua Umuhimu Wa Afya Na Kuahidi Kuendelea Kutoa Ushilikiano  Kwao  Na Kuwakaribisha Ndani Ya Jimbo Hilo Kupeleka Huduma Hiyo Muhimu Kwa Wananchi Wake.




Comments