Faiza afunguka ishu ya Zari kupata dili nchini



Msanii wa filamu nchini Tanzania, Faiza Ally huenda akawa ni moja ya mastaa ambao wamekasirishwa na kitendo cha mwanamama Zari kupata dili la kutangaza nepi za watoto za Soft Care.

Faiza Ally amesema kuwa ameshangazwa na kampuni hiyo kumtumia Zari kutoka Uganda kwenye matangazo yao ile hali kuna Watanzania wengi na wenye majina ambao wangetumika kutangaza bidhaa zao.

“I know this is gonna look bad for somepeople but let me be honest , how stupid Tanzanian can be , mastaa wote watanzania , watu wote watanzania hamkuona hata mmoja anae stahili kupata dili zaidi ya zari ? Ina maana uhitaji bongo umeisha mpaka tuweke watu kutoka nje ?? Kwa nini tunawapa kipa umbele wageni tunajizarau sisi ??? Mlishawahi kuona Uganda na kenya wamempa nani dili wakamuacha wa kwao ?? Eti sasa hivi mganda na mkenya wanapongezan na sisi wote tunaonekana hatukufaaa,“ameandika Faiza Ally kwenye ukurasa wake wa Instagram.


Hata hivyo, Faiza amemshangaa mwanamitindo Noel ambaye yeye ndiye aliyehusika kwa kiasi kikubwa kufanya connections hadi Zari kupata dili hilo.

“Noel you know all the Tanzania star na uko karibu hukuona anae faa ? I don’t hate zari but I hate kuona vitu wanavyo stahili kupata watanzania kapata mganda this is no good ! Hakuna nchi duniani utaenda ukaona mgeni anapewa kipa umbele zaidi ya mwenyeji , kiasi mpaka ukiwa unasuburi tax mpaka mwenye nchi apate na wewe ndio unafata,“ameeleza Faiza Ally.

Mtazamo wa Faiza umepigwa na baadhi ya Watanzania waliotoa maoni yao kwenye posti yake wakidai kuwa wanawake wengi wa Tanzania wanautumia umaarufu wao vibaya.

Jana Machi 28, 2018 Zari alisaini dili hilo nono la kutangaza bidhaa za Softcare Diapers ingawaje bado haijajulikana mkataba huo umemuingizia kiasi gani cha fedha.

Comments