FISI GUMZO KITWANA-SHINYANGA



Wakazi Wa Mtaa Wa Kitwana Kata Ya Busoka Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga Wameiomba Serikali Pamoja Na Uongozi Wa Kata Hiyo Kuwatatulia Changamoto Mbalimbali Zinazo Wakabili Ikiwa Ni Ulevi Wa Kupindukia Unaopelekea Upotevu Wa Vitu Mtaani Hapo Pamoja Na Kuvamiwa Na Fisi Katika Makazi Yao.

Wakizungumza Katika Mkutano Wa Hadhara Ulioitishwa Na Diwani Wa Kata Hiyo,Mh Julius Malale Shiganga,Wenye Lengo La Kujadili Maendeleo Ya Kata Hiyo Wamesema Changamoto Hizo Zinawarudisha Nyuma Kimaendeleo Hasa Suala La Ulevi Na Fisi Linapelekea Kufanya Shughuli Zao Kwa Kutojiamini Kwa Kuhofia Kuibiwa Na Kuliwa Na Wanyama hoa.

Kwa Upande Wake Mtendaji Wa Mtaa Huo Ndugu Sospeter Manyama Pamoja Na Mwenyekiti Wa Mtaa Huo Bwana Andrea Juma Wamekili Kuwepo Kwa Changamoto Hizo Na Kuwataka Wauza Pombe Kuacha Kufungua Virabu Asubuhi Kwani Wanapunguza Nguvu Kazi Ambapo Watu Wanakunywa Pombe Wakati Wa Kazi.


 Katika Hatua Nyingine Mtendaji Huyo Amewataka Wananchi Kuhudhuria Vikao Na Mikutano Inayoitishwa ili Kufahamu Vitu Vinavyozungumziwa Kuliko Kukaa Majumbani Kwao Na Kwenda Kwenye Ofisi Za Mtaa Kulalamika.

Naye Diwani Wa Kata Hiyo Mh Shiganga Amewataka Wananchi Hao Kuwa Na Subira  Na Kutokuwa Na Hofu Juu Ya Changamoto Hizo Kwani Amezifikisha Mahali Husika Na Zinafanyiwa Ufumbuzi.


Comments