NA MWANDISHI WETU
Zaidi ya wasichana Laki sita na Elfu
kuma na sita ( 616000 )wenye umri wa
miaka 9 mpaka 14 wilayani kahama mkoani shinyanga wanatarajiwa kupatiwa chanjo
ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
kwa mwaka huu 2018.
Yamebainishwa hayo na mkuu wa wilaya
hiyo bwana Fadhili Nkulu kwenye uzinduzi wa chanjo hiyo mpya ambapo kiwilaya umefanyika katika hospitali ya
wilaya kwa lengo la kuwakinga wasichana dhidi ya madhara mbalimbali ya kiafya
huku akiwataka viongozi wa serikali,kisiasa,dini,wananchi,wazazi na walezi
kuendelea kutoa elimu juu ya chanjo hiyo muhimu kwa jamii.
Kwaupande wake mratibu wa shughuli
za chanjo katika halmashauri ya mji wa
kahama bwana Mkola Vedasto amesema chanjo hiyo haina madhara ya aina yoyote kwa
mabinti hao hivyo wazazi na walezi wasiwe na hofu juu ya chanjo hiyo kwa watoto
wao.
Baadhi ya wasichana waliofika katika
uzinduzi huo kupatiwa chanjo hiyo wameuuliza maswali juu ya chanjo hiyo na
umuhimu wake kwa mratibu wa chanjo.
Nao wadau mbalimbali waliofika katika
zoezi hilo wakiwemo waalimu, manes na wafanyakazi wa idara mbalimbali
wameelezea jinsi ambavyo wameweza kufurahishwa na zoezi huku wakliahidi
kuendelea kuwa mabalozi wazuri juu ya kampeni hiyo muhimu.
INSERT
WALIMU.
Comments
Post a Comment