Sheria ya ndoa mwaka 1971 Yatajwa kuwa moja ya changamoto zinazochangia kuongezeka kwa ukatiri wa kijinsia Tarime



Imebainika kuwa sheria ya ndoa mwaka 1971 inakidhana na sheria ya mtoto  sura ya 21 ya mwaka  2009 ambayo inatetea haki haki za mtoto nakukinzana na sheria ya mwaka 1971 ambayo naruhusu mtoto WA miaka15 kuolewa kwa ridhaa ya wazazi suala ambapo linaendelea kupingwa na sheria za kimataifa

Sheria hiyo ambayo imedaiwa kuwa
Kuwa inaruhusu  watoto chini ya umri wa miaka 18 kuolewa imekuwa  ikichangia Kuongezeka kwa ukatiri  wa  watoto  ambapo watoto hao wamekuwa wakikosa haki zao za msingi kama vile kupata  Elimu

Hayo yamebainishwa na ostack Mligo wakili  kujitegemea kutoka shirika la KITUO cha msaada wa kisheria na haki za binadamu LSAC katika semina ya kuwajengea uwezo jeshi la polisi ikiwemo kitengo cha dawati la polisi Mkoa wa kipolisi Tarime Rorya iliyofanyika katika ukumbi wa  MCN Tarime

"inaeleza kama wazazi watakubaliana mtoto  Mwenye umri wa miaka 15 ataruhusiwa kuolewa na endapo kwa idhini ya mahakama  mtoto  Mwenye umri WA miaka 13 ataruhusiwa kuolewa pia,alisema  ostack

Aidha meneja mradi ATFGM Masanga Valeliani Mgani ameongeza kuwa mwaka huu ni mwaka wa  ukeketaji hivyo shirika hilo linalodhaminiwa na Terre des hommes  Netherland limeweza semina kwa ngaliba polisi wa kawaida,dawati la polisi,watendaji wa vijiji na kata ili kuhakikisha wanapatiwa ushauri na msaada kisheria

"Sisi mawakili tunatoa ushauri wa  kisheria kwa polisi kwa ajili ya kulinda mtoto  na mhanga yoyote wa haki za binadamu kwani jeshi la polisi pekee ndilo lenye nafasi kubwa ya kushughulikia haki za watoto,Alisema  Mligo

Pia mkuu wa  kituo  cha polisi Nyamwaga ameweza kuongeza kuwa Semina hiyo iliyotolewa na wataalamu hao itawasaidia katika utendaji kazi nakusema kuwa watatoa ushirikiano nakufanya kazi kwa ueledi ikiwemo kuzingatia sheria za nchi nakuwa hawatasita kutoa  msaada pindi wanapohitajika katika ushauri na maelekezo jambo ambalo  litasaidia kupunguza ukatiri WA kijinsia wilayani hapo.

"Mpaka sasa  ninavyozungumza nimepigiwa simu  kuwa kuna mtoto  amepigwa na mzazi wake vibaya hivo sisi kama polisi matatizo kama hayo yapo na tunaendelea kufanya ufumbuzi  kwa kukabiliana nayo  ili watoto wapate haki zao za msingi, Alisema, Fransis

Aidha mawakili pamoja na watumishi wameiomba serikali kubadili au kufanya marekebisho ya sheria hiyo jambo ambalo  litapelekea kuondokana na ukatiri unaotokana na kifungu hicho kuwabana wahusika wanaotetea haki za binadamu na kushindwa kutoa  haki kwa watoto.

Comments