chemical afunguka





Rapa wa kike nchini Tanzania, Claudia Lubao maarufu kama ‘Chemical’ amefunguka kuwa katika nyimbo zake zote wimbo wa ‘Mary mary’ ndio uliomtoa machozi kutokana na hali aliyokuwa nayo kipindi hicho.

Chemical amesema hayo kupitia KIKAANGONI inayorushwa kupitia ukurasa wa facebook ya EATV kuwa wimbo huo aliandika akiwa anatoka studio kurekodi na hakuwa na hali nzuri ya kimaisha.

“Mary mary ndio wimbo ambao nilikuwa naandika nimekaa barabarani nalia kutokana na hali niliyokuwa nayo sina hata mia natoka studio natembea nilipofika sehemu nikapumzika nikapata wazo nakuanza kuchora mistari ya ngoma hiyo”, amesema Chemical

Wimbo huo ambao baadhi ya mashairi yake yanaelezea namna ambavyo ameishi katika maisha ya kupambana na kutokata tamaa huku akiamini ipo siku atazifikia ndoto zake.

Comments