Harmonize amsifu Diamond baada ya ngoma yake kuweka rekodi ya pekee Tanzania




Msanii muziki Bongo, Harmonize amesema Diamond Platnumz amechangia kwa kiasi kikubwa ngoma yake ya Kwa Ngwaru kuweza kufika mbali zaidi.

Kauli ya muimbaji huyo inakuja mara baada ya wimbo huo kufikisha views milioni 10 katika mtandao wa YouTube kwa kipindi cha mwezi mmoja na kuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kufanya hivyo.

“Pia naamini uwepo wa Diamond umechangia kwa sababu ninaamini kuna sehemu muziki wangu haujafika, umefika kupitia Diamond pia,” amesema.

“So namshukuru ana mchango mkubwa licha ya verse ambayo amefanya kwenye wimbo lakini pia image yake imetumika kusaidia,” Harmonize ameiambia Wasafi TV.

Kwa Ngwaru ni wimbo wa pili kwa Harmonize kufanya na Diamond Platnumz baada ya kutoa wimbo unaokwenda kwa jina la Bado uliotoka miaka miwili iyopita.

Comments