Nora atamani kuolewa tena



Nuru Nasoro ‘Norah’

BAADA ya kuingia na kutoka kwenye ndoa kwa takriban mara mbili, mkongwe wa sinema za Kibongo, Nuru Nasoro ‘Norah’ amesema bado anatamani kuolewa tena kama itatokea amepata mtu sahihi.

Akipiga stori na mwanahabari wetu hivi karibuni kwa njia ya simu, Norah alisema licha ya kukutana na changamoto mbalimbali katika ndoa zake za awali na umri pia kuanza kumtupa mkono, bado akitokea mwanaume sahihi akamtangazia ndoa, atakubali.

“Naitamani ndoa kama atatokea mwanaume sahihi ambaye nitajiridhisha kwamba kweli ni mtu sahihi kwangu,” alisema Norah. Mrembo huyo alishawahi kuolewa na wanaume wawili tofauti na kujaaliwa kupata mtoto mmoja kabla ya kutengana nao.

Comments