- Get link
- X
- Other Apps
Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo bado ameendelea kuweka alama kwenye ramani ya soka barani Ulaya kwa kuvunja na kuweka rekodi lukuki za mpira wa miguu.
Kwa ushindi wa jana wa klabu yake dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa fainali ya klabu bingwa barani Ulaya unamfanya Ronaldo kuwa mchezaji wa kwanza barani Ulaya kuwahi kutokea kuchukua kombe la Klabu Bingwa mara tano.
Ronaldo amewaacha wakongwe wawili, Andrés Iniesta ambaye amechukua mara nne akiwa na Barcelona na kiungo wa zamani wa klabu ya AC Milan, Clarence Clyde Seedorf waliokuwa naye pamoja kwa kuchukua kombe hilo mara nne.
Comments
Post a Comment