- Get link
- X
- Other Apps
Uongozi wa timu ya Taifa ya Misri umethibitisha kuwa mshambuliaji wao hatari amabye anacheza kwenye klabu ya Liverpool, Mohamed Salah atashiriki kwenye michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi itakayoanaza kufanyika Juni mwaka huu.
Salah ambaye aliumia bega la kushoto wakati wa fainali ya klabu bingwa ya Ulaya Jumamosi iliyopita baada ya kuchezewa vibaya na Sergio Ramos na kutoka nje yauwanja dakika ya 24.
Kutokana na majeraha hayo yalileta wasiwasi kwa mashabiki na kuhusu kushiriki kwake kwenye michuano hiyo mikuba ya dunia.
Wakati huo huo Mwanasheria wa Misri, Bassam Wahba amesema amepeleka kesi kwenye shirikisho la soka duniani (FIFA) kumshtaki Ramos atoe kiasi cha Euro billion moja kwa kumuumiza makusudi Salah.
Comments
Post a Comment