- Get link
- X
- Other Apps
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee mwezi June tarehe 09 amealikwa kutumbuiza nchini Gabon mbele ya Rais wa nchi hiyo Ali Bongo.
Vanessa Mdee akizungumza na Bongo5 amesema kuwa kutakuwa na tamasha kubwa ambapo litahudhuriwa na wasanii wakubwa akiwemo mwanamuziki mashuhuri nchini humo, Frédéric Gassita na producer mkubwa wa muziki duniani, Humberto Gatica.
Mwaka jana Vanessa Mdee alikutana na Rais Ali Bongo wakati wakirekodi project ya The African Queens ya Ali Bongo na Frédéric Gassita.
Na kwenye project hiyo ya The African Queens kuna nyimbo, Vanessa Mdee kafanya na Rais Ali Bongo na huenda waka-perform kwenye jukwaa moja.
Rais Ali Bongo ni moja ya maproducer wakongwe wa muziki nchini humo na ameshatayarisha album nne za gwiji wa muziki nchini Gabon, Frédéric Gassita.
Comments
Post a Comment