Hatma ya Cristiano Ronaldo Madrid




Huenda Cristiano Ronaldo akaondoka  wakati huu wa majira ya joto baada ya Rais wa Real Madrid Florention Perez kuvunja ahadi aliyoiweka kwa nyota huyo.

Hii ni kutoka katika vyanzo vya habari vya Ureno ambavyo vinaeleza kwamba Ronaldo anajihisi kushushwa thamani na miamba hiyo ya La Liga.

Mkataba wa Ronaldo utamalizika Juni 2021 lakini kutokana na yeye kulipwa kidogo zaidi ya Lionel Messi wa Barcelona na Neymar wa Paris Saint-Germain.

Perez alimuahidi Ronaldo atakuwa mchezaji anayelipwa zaidi Ulaya baada ya ushindi katika fainali ya Ligi ya  Mabingwa wa Ulaya mwaka 2017 dhidi ya Juventus lakini hakuna ofa yoyote aliyoletewa.

Akiondoka Madrid, huenda akarudi Uingereza katika Klabu yake ya Amani ya Manchester United ambako aliondoka mwaka 2009,chaguo lingine ni PSG ambako inaripotiwa anaweza kubadilishwa na Neymar au pengine timu nyingine ambayo Ronaldo anaweza kwenda ni Juventus.

Comments